DRC

DRC ,,DARADHA MBILI MUHIMU ZA KATIKA UVIRA KIVU KUSINI NAKUPELEKEA UGUMU WA USAFIRISHAJI WA BIDHAA WA WATU .

FEBRUARI 27, 2024
Border
news image

Akazingumuza na MTV DRC ONLINE andre biadunia kiongozi wa mashirika ya kiraia katika mji wa Uvira asema kwa sasa hali ni mbaya kwa wafanya biashara na wakaazi wa Mkoa wa Kivu Kusini wanao ishi kusini mwa Bukavu baada ya Daraja Muhimu la Runengo ,Sange kukatika na kukata mawasiliano kati ya Mji wa Uvira na Bukavu ,kati ya Sange na Kabunambo kwani kwa sasa hakuna gari yoyote inayo pita kutokana na kukatika kwa daraja hizo muhimu.

Biadunia amesema Mito ilijaa na kubeba ardhi ilio kuwa ikishikilia daraja hizo ambazo ziliwekwa kwa serikali ya Mkoa miaka nne iliopita ,daraja ambazo tangu miaka kadhaa vilikuwa na matatizo wakaazi wakilalamika bila mafanikio yoyote kwa sasa hakuna njia nyingine isipokuwa kubeba mizigo kuvusha upande huu na mwengine kwa kutumia watu wabeba mizigo. Barabara hiyo ni muhimu kwamba inaunganisha Mji wa Bukavu na Mkoa wa Tanganyika,Taifa la Burundi na bandari la Uvira la Kalundu ambalo launganisha ,Tanzania,Zambia na Burundi .

Wakaazi wakiomba serikali kufanya jitihada zote kwakujenga daraja hizo ambazo sasa zitayumbisha uchumi na Maisha ya wakaazi kuwa magumu iwapo serikali haita shughulikia ujenzi huo kwa haraka .Congo ukiwa na shida za Barbara watu wengi wakitumia ndege kila mahali ,Taifa la Congo DRC ni kubwa lakini likikabiliwa na tatizo la maendeleo kutokana na ukubwa wake na serikali kuu ya kinshasa ikishutumiwa kutoshughulikia kwa haraka matati ya barabara za vijijini na mikoani .

Biadunia amesema watahakikisha wanasukuma serikali kuu ya Kinshasa kuhakikisha barabara hiyo inakarabatiwa hasa kuweka Daraja kwani kwa sasa hakuna Njia nyingine kwakusaidia wakaazi wa Uvira Kivu Kusini.

AM/MTV DRC ONLINEa